Create Yours

Top 120 Enock Maregesi Quotes (2025 Update)
Page 2 of 3

Enock Maregesi Quote: “Ubatizo ni toba iletayo ondoleo la dhambi. Mwangushe Goliati wa uzinzi katika maisha yako kwa kumtumia Yesu Kristo, ambaye ni Daudi wa mapandikizi yote ya dhambi katika maisha yetu.”
Enock Maregesi Quote: “Pesa ina maana kwa sababu ya wanawake.”
Enock Maregesi Quote: “Utajiri wa nje huwa unaanzia ndani, nao ni hekima.”
Enock Maregesi Quote: “Gluttony is the act of digging a grave with your own teeth.”
Enock Maregesi Quote: “Geuza hasira yako kuwa hekima.”
Enock Maregesi Quote: “Ukipata matatizo kumbuka kwamba Yesu alipata matatizo pia, na kutokana na matatizo hayo mimi na wewe tulipata uhuru. Soma Biblia. Soma nyimbo katika kitabu cha Zaburi zinazomsifu Mungu katika kipindi cha matatizo. Funga na kuomba ukiamini kwamba mapenzi ya Mungu kwetu ni huru, yasiyokuwa na masharti yoyote. Toa msamaha kwa waliokukosea. Ni kitu cha muhimu kujilimbikizia imani katika kipindi cha amani, ili matatizo yakitokea usiweze kuyumba.”
Enock Maregesi Quote: “Luka 22:20 ni mwisho wa agano la kale la damu za wanyama na mwanzo wa agano jipya la damu ya Yesu.”
Enock Maregesi Quote: “Ukitaka kumjua mwanamke jua historia yake.”
Enock Maregesi Quote: “Toa msamaha kwa waliokukosea kwa sababu dhambi zilizofanya mkosane zilitoka kwa Shetani.”
Enock Maregesi Quote: “Nuhu anasemekana kuwa mtu aliyedharaulika sana huko Babeli. Maisha yake yalijaa utata. Lakini ukweli ni kwamba, bila Nuhu mimi na wewe tusingekuwapo. Unayemdharau sana mwogope sana.”
Enock Maregesi Quote: “Kinachotokea katika dunia hii si kitu kizuri cha kuzoea au hata kufikiria. Hivyo tuna haki ya kuwa na mawazo, hasira na wanyonge kuhusiana na suala zima la maisha yetu hapa duniani. Hata hivyo hali hii itabaki kuwa hivyo kwa sababu Mungu ametaka iwe hivyo kwa sasa. Kwa maana hiyo, hekima ni kukubaliana na mapenzi ya Mungu. Lazima tukubaliane na kisichoweza kufikirika kuweza kubadilika.”
Enock Maregesi Quote: “Mungu alilibariki taifa la Israeli katika misingi ya kidini na si katika misingi ya kisiasa au misingi ya kihistoria; na asili ya dini ya Kikristo ni kutoka katika taifa hilo ambalo Biblia imelitaja kama taifa teule la Mwenyezi Mungu. Mgogoro wa Israeli na Palestina ulianzishwa na Israeli mwenyewe. Yakobo alipokea baraka iliyokuwa si ya kwake kwa kutumia hila ya Rebeka. Baraka ya Yakobo ilikuwa ya Esau.”
Enock Maregesi Quote: “Maamuzi ya Adamu na Hawa ya kutokumtii Mungu juu ya Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya, ndiyo yaliyosababisha Yesu Kristo ajitolee maisha yake ili wengine waweze kuishi. Hakuna Mungu bila Yesu. Mtafute Yesu, kukomboa sura na asili ya Mungu.”
Enock Maregesi Quote: “Kuzaliwa na kuishi ni mibaraka mikubwa ya Mwenyezi Mungu kuliko yote duniani.”
Enock Maregesi Quote: “Kama John Doe ana matatizo katika maisha yake acha ayatatue mwenyewe. Akishindwa atakuomba ushauri au ataomba ushauri kutoka kanisani kama ni Mkristo, au msikitini kama Mwislamu, au kutoka katika nyumba yoyote ya ibada kulingana na imani yake. Mtu akikuomba ushauri mshauri kwa moyo wako wote, wala usimshauri kwa unafiki au kinyongo cha aina yoyote ile.”
Enock Maregesi Quote: “Kushirikiana na maadui wa nchi yetu ni hatia ya kosa la uhaini. Adhabu yake ni kifo, au kifungo cha maisha.”
Enock Maregesi Quote: “Robert Louis Stevenson wa Uskochi aliponukuu nahau ya ‘kamera haiwezi kudanganya’ katika kitabu chake cha ‘South Seas’ mwaka 1896, miaka 57 baada ya sanaa ya upigaji wa picha kugunduliwa, hakumaanisha tuwe asili. Hakumaanisha tusizirekebishe picha zetu baada ya kuzipiga na kuzisafisha! Alimaanisha tuwe nadhifu tuonekanapo mbele za watu au mbele ya vyombo vya habari; ambapo picha itapigwa, itasafishwa, itachapishwa na itauzwa kama ilivyo bila kurekebishwa.”
Enock Maregesi Quote: “Mojawapo ya misingi ya ujasusi ni kuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya unachojua, usichojua na unachofikiria. Unaweza kusema unajua wakati hujui. Maamuzi yasiyo sahihi ya kijasusi huweza kuiletea tume madhara makubwa.”
Enock Maregesi Quote: “Kila mtu anapaswa kuwa na siri angalau moja katika maisha yake.”
Enock Maregesi Quote: “Katika jiji la Dar watu hawaendi kazini. Wanakwenda vitani. Wania kilicho chako ukidhulumiwa. Utajiri humpendelea anayejaribu.”
Enock Maregesi Quote: “Acha alama katika dunia baada ya kuondoka.”
Enock Maregesi Quote: “There are many internal secrets that make a person continue to succeed, and there are many external secrets that make a person continue to hide their secrets. Internal secrets are true secrets, while the outer secrets are false secrets, aimed at hiding the truth. However, the secret to success is hard work, knowledge and secrecy.”
Enock Maregesi Quote: “Success is a test.”
Enock Maregesi Quote: “Kiswahili ni lugha rasmi ya nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Ni lugha isiyo rasmi ya nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Lugha ya Kiswahili ni mali ya nchi za Afrika ya Mashariki, si mali ya nchi za Afrika Mashariki peke yake. Pia, Kiswahili ni lugha rasmi ya Umoja wa Afrika; pamoja na Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kireno na Kihispania. Kiswahili ni lugha inayozungumzwa zaidi nchini Tanzania kuliko nchi nyingine yoyote ile, duniani.”
Enock Maregesi Quote: “Yesu wakati anakufa msalabani hakufikiria kifo. Alifikiria maisha.”
Enock Maregesi Quote: “Kukiuka Amri Kumi za Mungu si dhambi ni matawi ya dhambi. Dhambi ni kumkana Mungu na kumkubali Shetani.”
Enock Maregesi Quote: “Ukitaka kufanikiwa katika maisha angalia watu wanataka nini halafu wape. Kama wanataka burudani wape. Kama wanataka elimu wape. Kama wanataka bidhaa wape. Kama wanataka huduma wape. Wape kwa msaada wa wataalamu.”
Enock Maregesi Quote: “Ukitaka watu wakuheshimu usitumie mabavu. Tumia hekima. Maana, watu hawaheshimu wewe ni nani au unatoka wapi, wanaheshimu nguvu ya matendo yako. Kama una tatizo na mtu usichukue uamuzi wa haraka. Ongea na watu kupata hekima.”
Enock Maregesi Quote: “Mungu alisema tupendane katika shida na raha; Luka 6:27-36. Katika matatizo mpende hasimuyo. Maumivu ya watu hufanana.”
Enock Maregesi Quote: “Ukiwa mchapakazi hodari mwenye msimamo na nia thabiti ya utendaji kazi unaweza kuwa mpweke kwa maana ya kuwa na marafiki wachache. Lakini mashabiki utakuwa nao wengi.”
Enock Maregesi Quote: “If a leader for the right reasons is blessed by God, even the people he leads will be blessed by God as well. But if the leader is cursed by God because of iniquity, even the people he leads will be cursed as well.”
Enock Maregesi Quote: “Mungu akikubariki kipaji chako watu watasema ni laana. Maisha yako ni sawa na mto. Unakoelekea ni baharini. Lakini sasa umefika kwenye mlango wa bahari. Unahangaika upite wapi kufika baharini, ambapo utaogelea kwa kadiri utakavyoweza. Utakapofika baharini, watu, badala ya kusema umebarikiwa, watasema umelaaniwa, badala ya kukuita malaika, watakuita shetani. Mafanikio hayapimwi kwa pesa au mali kiasi gani unayo, mafanikio yanapimwa kwa amani ya moyo au maisha ya watu kiasi gani umeboresha.”
Enock Maregesi Quote: “Baraka inapotoka kwa Mungu lengo lake ni kukufanya umpende Mungu kupitia wenzako.”
Enock Maregesi Quote: “Lengo kuu la Shetani kuingilia uumbaji wa Mungu kwa kutumia Succubus na Incubus ni kumzuia Yesu asirudi kwa mara ya pili. Anajua akiingilia uumbaji huo na kuwafanya watu wote wawe na roho za kishetani, wokovu hautakuwa na maana, Yesu hatakuwa na mtu wa kumwokoa atakaporudi kwa mara ya pili.”
Enock Maregesi Quote: “We are the children of Nelson Mandela; we are the children of Kwame Nkrumah; we are the children of Haile Selassie; we are the children of Samora Machel; we are the children of Robert Mugabe; we are the children of Patrice Lumumba; we are the children of Julius Kambarage Nyerere. We know who we are.”
Enock Maregesi Quote: “Kipimo cha hofu ya Mungu ni kumjua!”
Enock Maregesi Quote: “Kama Mungu na Shetani hawako ndani yako, hiyo vita ya kiroho unaipigania wapi?”
Enock Maregesi Quote: “Heri kuwa Mkristo wa Yesu Kristo, au Mwislamu wa Mtume Muhammad, kuliko kuwa mkristo wa kanisa au mwislamu wa msikiti.”
Enock Maregesi Quote: “Mahatma Gandhi alipigwa risasi na kufariki dunia baada ya maisha yake kumfelisha. Lakini kifo chake kiliipatia India uhuru kutoka Uingereza. Hivyo, akafanikiwa.”
Enock Maregesi Quote: “Words are the bricks of our world and they have the power to change it.”
Enock Maregesi Quote: “Jina la Yesu ni kubwa kuliko majina yote duniani na hata kuzimu. Lazima Shetani aliogope kuliko anavyomwogopa Bikira Maria au sakramenti za aina zote. Kumbuka, jina la Yesu halitajwi kilingeni. Linatajwa kanisani, ambapo linatajwa kinafiki. Hivyo, aliye na mamlaka ya kuaminiwa na kuabudiwa na aponyaye ni Yesu Kristo peke yake.”
Enock Maregesi Quote: “Kitabu cha ‘Kolonia Santita’ ni kitabu cha wasomi na wasiokuwa wasomi, watu wa mijini na watu wa vijijini, watu wazima, vijana na watoto. Hadhira ya kitabu hiki ni jamii nzima ya Tanzania.”
Enock Maregesi Quote: “Wakati ndege inapaa huwa inapambana na upepo. Lakini inapaa, hata hivyo.”
Enock Maregesi Quote: “Kama utafiti wa mtu umevuka mipaka ya ukweli au uhalisia toa utafiti mwingine kuupinga huo wa kwake, kwa lengo la kuelimisha wengi. Haina maana kusema jambo si la kweli na usitwambie kwa nini si la kweli.”
Enock Maregesi Quote: “I have written all the 406 pages of my book in Swahili words. Even the countries are in Swahili. Instead of ‘Nigeria’, for example, I have written ‘Nijeria’. That is how it is written in the Swahili dictionary. This can seem as a minor detail and that people may find my mission close to ridiculous! However, single letters and commas matter.”
Enock Maregesi Quote: “Watu wakikuonyesha tabia zao za ndani kabisa waamini. Wanajijua vizuri zaidi, kuliko unavyowajua.”
Enock Maregesi Quote: “Ujasusi ni kitu cha muhimu kwa maendeleo ya nchi yoyote. Watu wanaoshughulika na ujasusi wanapaswa kuwa makini mno kwani kazi yao ni nyeti sana kulinganisha na kazi za watu wengine. Kosa dogo la kiusalama linaweza kubadili mwelekeo wa historia ya nchi.”
Enock Maregesi Quote: “Jambazi aliyekubuhu hawezi kumuua mtu bila kumwambia kwa nini anamuua. Si sheria ya John Murphy. Ni sheria ya EAC.”
Enock Maregesi Quote: “Mwisho wa sura si mwisho wa kitabu. Fungua ukurasa mwingine.”
Enock Maregesi Quote: “Mpenzi. Sikiliza. Magaidi yaliyomuua Marciano yana mtandao dunia nzima na watu wote wanayajua. Yanaitwa Kolonia Santita. Tatizo hata hivyo ni moja: Hakuna mtu amewahi kuthibitisha au kutoa ushuhuda wa uhalifu wao ili watiwe nguvuni. Huendesha maisha yao kibabe na yana kila mbinu ya kukwepa sheria, ndani na nje ya Meksiko. Watu wengi wameuwawa kwa sababu ya Kolonia Santita. Ukileta kidomodomo yanakuua; au yanakupa notisi ya kuhama mji au nchi, ukakae mbali na Meksiko au Mexico City.”
PREV 1 2 3 NEXT
Motivational Quotes
Inspirational Entrepreneurship Quotes
Positive Quotes
Albert Einstein Quotes
Startup Quotes
Steve Jobs Quotes
Success Quotes
Inspirational Quotes
Courage Quotes
Life Quotes
Focus Quotes
Swami Vivekananda Quotes

Beautiful Wallpapers and Images

We hope you enjoyed our collection of 120 Enock Maregesi Quotes.

All the images on this page were created with QuoteFancy Studio.

Use QuoteFancy Studio to create high-quality images for your desktop backgrounds, blog posts, presentations, social media, videos, posters, and more.

Learn more