Create Yours

Top 120 Enock Maregesi Quotes (2025 Update)
Page 3 of 3

Enock Maregesi Quote: “Ukiwapa watu kile wanachokitaka wataendelea kukihitaji.”
Enock Maregesi Quote: “Mungu anatupenda sana, ndiyo maana akamleta Mwanawe wa pekee ili afe kwa ajili yetu, lakini haupendi mfumo wa maisha wa dunia hii.”
Enock Maregesi Quote: “Kula kwa kiasi.”
Enock Maregesi Quote: “Ukitaka kuwa na mashabiki fanya kitu ambacho si cha kawaida katika maisha yako, kila siku.”
Enock Maregesi Quote: “Kila kipato kina mashetani yake, mengine mazuri na mengine mabaya, lakini mengi ni mabaya. Wakati mwingine maskini ahitaji pesa, pesa anaweza kushindwa kuidhibiti, anahitaji paa na kuta nne kujisetiri yeye na familia yake.”
Enock Maregesi Quote: “Mbili jumulisha mbili wakati mwingine si sawa na nne. Ni sawa na nne jumulisha moja kwa sababu moja ni nguvu ya ushirikiano.”
Enock Maregesi Quote: “Serikali inayodhulumu wananchi wake ni hatari kuliko simba.”
Enock Maregesi Quote: “Ukiona kitu ambacho hukupaswa kuona, au ukisikia kitu ambacho hukupaswa kusikia, fumba macho kwa kuyakodoa! Ulichokiona au kukisikia usikiseme leo na hata milele. Jifanye hukuona kitu, hukusikia kitu. Ukifumbua macho kwa kuyakodoa utapata matatizo, makubwa.”
Enock Maregesi Quote: “Ajali haina mkanda. Punguza mwendo wa gari lako.”
Enock Maregesi Quote: “Kwa sababu ya udadisi wa hali ya juu nasoma kila kitu ninachokutana nacho hasa vile visivyonipendeza. Ukitaka kupata maarifa usisome tu vitabu vinavyokupendeza. Soma vitabu visivyokupendeza.”
Enock Maregesi Quote: “Imani ni nia ya kujua kisichoweza kujulikana na hupeleka watu kwenye ukweli. Kuamini hupotosha, na ni nia ya kudharau kinachoweza kujulikana.”
Enock Maregesi Quote: “Kufanikiwa katika maisha lazima kitu fulani ambacho si cha kawaida kitokee katika maisha yako, bila kujali uko upande wa Yesu au upande wa Shetani. Kufanikiwa katika maisha ni sawa na kwenda mbinguni, au kuishi mbinguni duniani. Kitu ambacho si cha kawaida kutokea katika maisha yako ni sawa na kifo. Fanya kitu ambacho hujawahi kufanya kupata kitu ambacho hujawahi kupata.”
Enock Maregesi Quote: “Wazazi wetu ni watu wa kuheshimu kuliko kitu kingine chochote kile kwa sababu wana uwezo wa kuona tusipoweza kuona. Yaani, wanajua kilichokuwepo kabla ya sisi kuzaliwa na wanajua kilichokuwepo baada ya sisi kuzaliwa. Maisha tuliyopitia, wazazi wetu walishapitia. Tulipokuwa, wazazi wetu walishakuwepo; na tulichofanya, wazazi wetu walishafanya. Hivyo, hatuna budi kuwaheshimu wazazi wetu. Lakini, wazazi wetu wanapaswa kujiheshimu kutufundisha adabu na maadili mema.”
Enock Maregesi Quote: “Kama unataka kuijua vizuri historia ya mwanamke hasa mwanamke unayetaka kuoana naye, usifanye naye mapenzi kwa miezi sita angalau. Ukifanya naye mapenzi kwa miezi sita au zaidi, au ndani ya miezi sita, halafu akakuchanganya kimapenzi, hutakuwa na uwezo mkubwa wa kuwasikiliza watu kuhusiana na historia yake.”
Enock Maregesi Quote: “Toa msaada katika jamii iliyosaidia kukulea ulipokuwa mdogo.”
Enock Maregesi Quote: “Katika maisha watu watakufitini, watakurubuni na watakukatisha tamaa. Sema hapana kwa ndiyo nyingi.”
Enock Maregesi Quote: “Chukia kushindwa, zaidi ya unavyofurahia kushinda.”
Enock Maregesi Quote: “Lakini Kiswahili kilizaliwa Afrika Mashariki. Kwa nini hatuithamini lugha yetu? Kwa nini hatuzithamini lugha zetu za makabila? Kwa nini hatuipendi na kuitetea lugha yetu ya taifa ambayo ndiyo lugha ya biashara na mawasiliano ya Afrika Mashariki? Kwa nini hatuvitetei vizazi vijavyo kwa kuvitetea vizazi vya leo?”
Enock Maregesi Quote: “Watu wa kulisaidia bara la Afrika hawatatoka Amerika au kwingineko. Afrika ni tatizo letu. Watatoka Afrika kwenyewe.”
Enock Maregesi Quote: “Kuwa makini na kila kitu unachofanya kwa maana ubongo ni kitu cha ajabu, ubongo una uwezo wa kukupotosha.”
Enock Maregesi Quote: “Wajerumani, hata hivyo, wakati wa utawala wao waliruhusu Kiswahili kiwe lugha halisi ya taifa nchini Tanzania kwa vile hawakukiongea Kiingereza wala hawakukipenda. Ndiyo maana Kiswahili kinazungumzwa zaidi nchini Tanzania kuliko Kenya au Uganda.”
Enock Maregesi Quote: “Mungu anaweza kusamehe kutokujua kwetu kwa sababu hatuwezi kukiamini kile tusichokijua; na hata kama tutaweza kuadhibiwa kwa kile tusichokijua, hatutaweza kuadhibiwa vikali kama ambavyo tutaweza kuadhibiwa kwa kile tunachokijua.”
Enock Maregesi Quote: “Bila Masihi hakuna atakayetunukiwa tiketi ya kuingia katika ufalme wa Mungu, kwa sababu hakuna atakayeokolewa bila Masihi.”
Enock Maregesi Quote: “Watanzania wengi hawana mzuka na kazi, ndiyo maana wanashindwa.”
Enock Maregesi Quote: “Kama una akili kuwa kawaida. Kama una nguvu kuwa mkarimu. Kama una pesa kuwa mnyenyekevu. Ukitaka kuwa na akili kuwa kawaida. Ukitaka kuwa na nguvu kuwa mkarimu. Ukitaka kuwa na pesa kuwa mnyenyekevu.”
Enock Maregesi Quote: “Without true opposition the country can not be ruled, although it can be dominated without true opposition. To be ruled is to accept to be dominated; to be dominated is to accept to be ruled. Without true opposition there is no true patriotism; without true patriotism there is no true opposition. Be a true opponent of the government, by being a true patriarch of your country; defend your country from the heart, on the fundamental issues of the country’s constitution.”
Enock Maregesi Quote: “Lolote unalolifikiria yupo mtu mahali fulani duniani ameshalifikiria.”
Enock Maregesi Quote: “Ukiua mtu bila kumwambia kwa nini unamuua anaweza kujua umemuua kwa kumwonea. Akijua umemuua kwa kumwonea roho yake inaweza kukusumbua wewe na familia yako maisha yenu yote. Makachero wa EAC wana leseni ya kuua. Lakini si kuua ovyo kama James Bond. Kila wanayemuua lazima waandike ripoti kwa nini wamemuua. Kachero wa EAC akiua mtu, kwa makosa, kwa bahati mbaya, atalindwa na Mwenyezi Mungu. Atalindwa na Tambiko la Tume ya Dunia.”
Enock Maregesi Quote: “Ramachandra maana yake ni mwezi. Mwezi ni setilaiti na mwezi unamulika. Ramachandra anaitwa setilaiti kwa sababu ya umuhimu wake katika bara la Asia. Anamulika India na bara zima la Asia, na Australia, kwa niaba ya Kolonia Santita. Ana miaka 44. Ana mke na watoto 6. Ni jambazi aliyekubuhu wa India.”
Enock Maregesi Quote: “Mwili wako una uwezo wa kujua kabla yako kitakachotokea baadaye. Kama una njaa kwa mfano, mwili wako utakwambia. Kama una kiu, mwili wako utakwambia. Kama unaumwa, mwili wako utakwambia. Kama kuna kitu kibaya kinatarajia kutokea katika maisha yako au katika maisha ya mtu mwingine, mwili wako utakwambia. Kuwa makini na alamu zinazotoka ndani ya mwili wako, kwani hizo ni ishara za Roho Mtakatifu kukuepusha na matatizo ya dunia hii.”
Enock Maregesi Quote: “Kadiri unavyozidi kupanda juu ndivyo utakavyoanguka vibaya.”
Enock Maregesi Quote: “Mungu hagawi pesa kwa watu kama watu wanavyofikiria. Anagawa upendo na hekima.”
Enock Maregesi Quote: “Mungu alikupa maisha akakupa akili ili utambue jema na baya na akakupa amri zake ili uishi kwa amani na upendo. Kama Mungu hayupo mwanamume na mwanamke walitoka wapi? Wazazi wako walitoka wapi? Wazazi wao walitoka wapi? Wazazi wao walitoka wapi?”
Enock Maregesi Quote: “Ukiua mtu damu yake itakusuta maisha yako yote! Itaongea na wewe ikikulaumu milele!”
Enock Maregesi Quote: “Kupata maarifa kutokana na shida ni jambo la kawaida, lakini kupata maarifa bila shida ni hekima.”
Enock Maregesi Quote: “People think that other international languages are smarter and more business wise. But they have to understand that we have to preserve our culture.”
Enock Maregesi Quote: “Kitu cha kwanza kufanya kama umeamua kuficha ukweli wape watu ukweli mwingine kulinda thamani ya utu wako.”
Enock Maregesi Quote: “Write as much as you can. Read as much as you can. Use the library and the internet carefully for research and talk to people about things that matter. If you have an idea in your head talk it to people as a normal conversation, to get their natural opinions. And don’t forget to jot down discreetly any new ideas you get from people. God may use other people to convey messages to you, that may add more information to the ideas you already have.”
PREV 1 2 3 NEXT
Motivational Quotes
Inspirational Entrepreneurship Quotes
Positive Quotes
Albert Einstein Quotes
Startup Quotes
Steve Jobs Quotes
Success Quotes
Inspirational Quotes
Courage Quotes
Life Quotes
Focus Quotes
Swami Vivekananda Quotes

Beautiful Wallpapers and Images

We hope you enjoyed our collection of 120 Enock Maregesi Quotes.

All the images on this page were created with QuoteFancy Studio.

Use QuoteFancy Studio to create high-quality images for your desktop backgrounds, blog posts, presentations, social media, videos, posters, and more.

Learn more