Create Yours

Top 120 Enock Maregesi Quotes (2025 Update)

Enock Maregesi Quote: “Your dreams won’t die until you die don’t ever stop believing!”
Enock Maregesi Quote: “Mapenzi ni wazimu, kama si wazimu si mapenzi.”
Enock Maregesi Quote: “Mwambie mtoto wako maneno mazuri anapokuwa ananyonya na kukuangalia machoni kwa kukukodolea. Maneno utakayomwambia ndiyo yatakayokuwa msingi wa mawazo yake, na ndiyo yatakayoumba maisha yake atakapokuwa mkubwa.”
Enock Maregesi Quote: “Kitu kikishindikana katika maisha yako kamwe usikate tamaa kwa sababu kushindwa ni mama wa mafanikio na kukata tamaa ni mama wa kushindwa.”
Enock Maregesi Quote: “Maisha tunayoishi ni mafupi, maisha ya mbinguni ni ya milele. Fundisha familia yako upendo na hofu ya Mungu, kwani hiyo ndiyo akili kushinda zote. Hekima ya kutunza familia inapatikana katika kitabu cha Mithali cha Agano la Kale.”
Enock Maregesi Quote: “Usikate tamaa juu ya ndoto zako.”
Enock Maregesi Quote: “Kufanikiwa katika maisha lazima usimamiwe na nguvu za nuru au nguvu za giza. Kama ni nuru lazima ubobee katika nuru. Kama ni giza lazima ubobee katika giza.”
Enock Maregesi Quote: “Kuishi na watu vizuri ni ufundi mkubwa.”
Enock Maregesi Quote: “Hakuna mtu mwenye akili timamu anayetaka mabaya katika maisha yake. Mwanamume atake mwanamke mwenye matendo mema. Mwanamke atake mwanamume mwenye matendo mema. Misingi ya hasanati ni misingi ya utu. Tukiishi katika misingi ya utu, misingi ya matendo mema, tutaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu. Kila mtu anapaswa kuishi na mke au mume aliye mwema.”
Enock Maregesi Quote: “Ukarimu ni bora kuliko hekima, na kulitambua hilo ndiyo mwanzo wa hekima.”
Enock Maregesi Quote: “Heshima hujengwa kwa hekima, haijengwi kwa misuli.”
Enock Maregesi Quote: “Mungu ni mwingi wa hekima, lakini kwa nini alimuumba Shetani? Kwa sababu, Shetani wakati mwingine ni hekima. Ukiendelea kupigwa, bila wewe kupiga, unaweza kuumia, familia yako inaweza kuumia pia! Kuepusha matatizo ya familia yako, wakati mwingine unahitaji kupigana.”
Enock Maregesi Quote: “Andika Kiswahili vizuri. Wala usiogope kuonekana mshamba. Kwa sababu unachokifanya hasa ni kwa ajili ya vizazi vijavyo.”
Enock Maregesi Quote: “The best weapon for selfishness is selfishness for the cause of others.”
Enock Maregesi Quote: “Usipokula maisha maisha yatakufanya chakula.”
Enock Maregesi Quote: “Ijapokuwa maombi ya sifa yana nguvu kuliko maombi ya kushukuru, kushukuru kuna nguvu kuliko kuomba.”
Enock Maregesi Quote: “Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa baba kwa familia yake. Kwa Tanzania alikuwa mlezi; wa ndoto ya haki, amani, uzalendo, ujamaa, na uhuru.”
Enock Maregesi Quote: “Maskini hufundisha watoto wake jinsi ya kupambana na maisha. Tajiri hufundisha watoto wake jinsi ya kuwa matajiri.”
Enock Maregesi Quote: “Usimdharau mtu aliyesaidia kukupa kazi ulipokuwa huna kazi, wala usimdharau mtu aliyesaidia kukulea ulipokuwa mdogo, au mtu aliyeokoa maisha yako au mtu aliyekusaidia kwa namna yoyote ile. Ukimdharau, utakaposhuka, atakusaidia kwa rehema za Mwenyezi Mungu.”
Enock Maregesi Quote: “Hasanati ni matendo mema. Mema yanatoka kwa Mungu. Mabaya yanatoka kwa Shetani. Mke mwema anatoka kwa Mungu. Mke mbaya anatoka kwa Shetani. Mke mwema ana hekima na busara, ana maadili na tabia njema, ana utu na uchapakazi, ana wema na upendo, na ana aibu kwa wanaume.”
Enock Maregesi Quote: “Katika maisha ni vigumu kupata jibu sahihi kwa akili yako mwenyewe.”
Enock Maregesi Quote: “Your mind wants to succeed, but your life does not want; how will you succeed? Success is not an easy thing! Success is allergic to laziness! However, it is amenable to intelligence and diligence.”
Enock Maregesi Quote: “Mama anaweza kufa ili mwanawe aishi, anaweza kufunga na kuomba ili mwanawe Mungu amsaidie ashinde mtihani wake, anaweza kulala njaa ili mwanawe ale, anaweza kujitolea vitu vingi au mambo mengi katika maisha yake ili mwanawe aishi vizuri, anaweza kuingia dhambini ili mwanawe asamehewe.”
Enock Maregesi Quote: “Usiingilie mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu. Kuingilia mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu ni dhambi. Dhambi hiyo itakuathiri. Hivyo, jali mambo yako – ya mwingine Mungu anayafanyia kazi – hadi utakapoitwa na Mungu kuingilia kati. Kuingilia kati mambo ya mtu mwingine kunaweza kuathiri mpango wa Mungu katika maisha yake. Hivyo, acha.”
Enock Maregesi Quote: “Nimebadili utaratibu wangu siku hizi kutokana na maadili ya watoto wetu. Siongei na watoto wangu kuhusu Mungu. Naongea na Mungu kuhusu watoto wangu. Yesu alilipa gharama ya maisha yake kutununua kutoka kwa Shetani. Tumrudie; hususan katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa.”
Enock Maregesi Quote: “Kwa nini Biblia imejaa mafumbo? Biblia imejaa mafumbo kwa sababu akili za watu bado hazijakomaa kuupokea ukweli. Yesu na waandishi wote wa Biblia waliongea na kuandika kimafumbo, ili Neno la Mungu lijidhihirishe lenyewe kiroho katika mawazo ya mtu.”
Enock Maregesi Quote: “Ukikosana na mwanamke usimpige mchana. Mpige usiku. Ukimpiga mchana watu watasema umemwonea. Ukimpiga usiku watu watasema huenda alikuwa na makosa. Wanawake hawatakiwi kupigwa.”
Enock Maregesi Quote: “Usisubiri Mungu afanye kitu ambacho Mungu anasubiri ufanye.”
Enock Maregesi Quote: “To be able to influence Tanzanian literature and African literature, and sell our books in Tanzania as well as in our continent, we need to be committed to what we do. And what we do is writing. Write as much as you can. Read as much as you can. Use the library and the internet carefully for research and talk to people, about things that matter. To make a living from writing, and make people read again in Tanzania and Africa; we must write very well, very good stories.”
Enock Maregesi Quote: “Watu hubariki wenzao ambao ni wakarimu, na hulaani wenzao ambao ni wabahili. Ukiwa mkarimu kwa watu umekopa neema kutoka kwa Mungu, na Mungu atakulipa kutokana na matendo yako.”
Enock Maregesi Quote: “Ukiwanyima watoto uhuru wa kuwa watoto leo watakuwa na uhuru wa kuwa watoto kesho.”
Enock Maregesi Quote: “Ningependa – maisha yangu yatakapokoma hapa duniani – kukumbukwa kama mtu aliyejitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote, kutumia kipaji alichopewa na Mungu.”
Enock Maregesi Quote: “Maombi ya sifa huunganisha watu wa Mungu na hutayarisha njia kwa ajili ya uwezo wa Mungu katika maisha yetu. Thamani ya maombi ya sifa wakati wa matatizo ni kuimarisha imani yetu, na kuwa karibu na Mungu wetu. Mungu anataka tumpe sifa na kumshukuru kwa kila jambo, kama Mtume Paulo anavyosema katika waraka wa kwanza wa Wathesalonike 5:16-18. Kumshukuru Mungu wakati wa matatizo ni amri, si ombi.”
Enock Maregesi Quote: “Kupata maarifa kutokana na shida ni jambo la kawaida maana shida ni kipimo cha akili, lakini kupata maarifa bila shida ni hekima maana hekima ni ufunguo wa maamuzi mema na udadisi wa kiakili.”
Enock Maregesi Quote: “Mwaka mmoja na nusu unatosha kumjua mwanamke kabla ya ndoa. Miezi sita itakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mchumba. Mwaka mmoja na nusu utakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mke.”
Enock Maregesi Quote: “Kafara ya maombi ni kushukuru wakati wa matatizo. Kushukuru kuna nguvu kuliko kuomba.”
Enock Maregesi Quote: “Hekima ni fikra inayotoka moyoni, busara ni hekima inayozungumzwa.”
Enock Maregesi Quote: “Watu hawaheshimu wewe ni nani au unatoka wapi. Wanaheshimu nguvu ya matendo yako.”
Enock Maregesi Quote: “Mungu hutumia majaribu makubwa katika maisha yetu kutukomaza na kutukamilisha. Kitu kisichokuua hukufanya mpiganaji.”
Enock Maregesi Quote: “Kama umefanya au umesema kitu kibaya na ukasema ukweli mbele ya mtu au ya watu, omba msamaha kupata tena kibali cha umma.”
Enock Maregesi Quote: “Secure tomorrow today by sowing good seeds today and by watering them with faith and love to others.”
Enock Maregesi Quote: “Behave professionally and let any bad feelings out of life!”
Enock Maregesi Quote: “Wakati mwingine unakokwenda siko. Rudi nyuma. Ukirudi nyuma huko nyuma ndiko mbele yako.”
Enock Maregesi Quote: “Watu wakikuonyesha tabia zao za ndani kabisa usisubiri wakuonyeshe tena ndiyo uwaamini. Waamini kwa mara ya kwanza. Mtu, kwa mfano, akionyesha kwa mara ya kwanza kuwa si mwaminifu mwamini. Anajijua zaidi kuliko unavyomjua. Aidha, mtu akikwambia anakupenda halafu akakupiga ni mnafiki. Maneno yake yatasema anakupenda, vitendo vyake vitasema hakupendi. Ukiwa makini na matendo ya mtu, si maneno yake, utamjua. Sikiliza maoni ya watu! Kuwa makini na matendo ya mtu.”
Enock Maregesi Quote: “Amani ya nafsi ni zaidi ya amani ya kisiasa. Amani ya kisiasa itaweza kupatikana endapo watu watakuwa na amani ndani ya mioyo yao. Watu wakiithamini amani na kuielewa watayafurahia maisha yao, na mataifa yakiithamini amani na kuielewa yatastawi. Vita hutengenezwa ndani ya mioyo ya watu. Ukiitafuta amani ndani ya moyo wako, taifa halitasimama kupigana na taifa, amani itaweza kupatikana.”
Enock Maregesi Quote: “Kuna maisha baada ya saa tisa na nusu. Kuwa makini na raia.”
Enock Maregesi Quote: “Maskini mwenye pesa nyingi ni tajiri bahili. Tajiri mwenye mifuko iliyotoboka ni tajiri badhiri.”
Enock Maregesi Quote: “Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka wazi kwamba unapomsamehe mtu, huwezi kupotezea au kukana uzito wa kosa alilokufanyia. Kusamehe ni hali fulani inayotoka ndani ya moyo wa mtu, ikiwa na hali ya uhuru wa hiari wa mtu mwenyewe kuamua kuachilia kile kinachomuumiza, pasipo kuwepo masharti ya aina yoyote ile kwa mtu aliyemuumiza.”
Enock Maregesi Quote: “Maisha yangu ni darasa. Jifunzeni kutokana na maisha yangu, jifunzeni kutokana na sifa zangu za ushupavu, jifunzeni kutokana na sifa zangu za udhaifu, kutatua matatizo katika maisha yenu.”
Enock Maregesi Quote: “Wape watoto wako urithi wa kutosha ili waweze kufanya kitu, lakini si urithi wa kutosha ili wasiweze kufanya kitu. Wape watoto uhuru wanaostahili kupata, uhuru wa mahesabu, lakini si uhuru wa kila kitu.”
PREV 1 2 3 NEXT
Motivational Quotes
Inspirational Entrepreneurship Quotes
Positive Quotes
Albert Einstein Quotes
Startup Quotes
Steve Jobs Quotes
Success Quotes
Inspirational Quotes
Courage Quotes
Life Quotes
Focus Quotes
Swami Vivekananda Quotes

Beautiful Wallpapers and Images

We hope you enjoyed our collection of 120 Enock Maregesi Quotes.

All the images on this page were created with QuoteFancy Studio.

Use QuoteFancy Studio to create high-quality images for your desktop backgrounds, blog posts, presentations, social media, videos, posters, and more.

Learn more